Utazaa Mtoto Wa Kipekee: You Will Give Birth To A Special Child (Swahili)

Utazaa Mtoto Wa Kipekee

Ni tabia ya Mungu ya kwamba, akiwa na kitu muhimu anachotaka kukutendea, anazunguka ili adui zako waonekane kama wako mbele yako na wewe ukionekana kama uko nyuma sana. Mara nyingine unaweza kuona kama Mungu  ameshakusahau au amekuacha lakini, wakati wa Mungu ni tofauti na wakati wa watu, kwa sababu Mungu anatenda mambo yake katika nguvu zake nyingi. Biblia linasema Elkannah alikuwa na wake wawili, Hannah na Penina. Hannah haakuwa na mtoto, Penina alikuwa nao.


Tena Peninah alikuwa mke wa pili aliyekuja baada ya Hannah lakini sasa anaonekana kama anafaidika sana katika maisha wakati Hannah analia machozi kila siku. Neno la Mungu linasema Penina kila siku alimdharau Hannah kwa sababu ya kutokuwa na mtoto.

Pregnancy
Ndugu yangu labda upo katika hali kama ya Hannah leo, nimekuja na neno kwako, ‘utazaa mtoto wa kipekee'. Mungu akitaka kutenda mambo makuu kwako, ni tabia yake ya kuwatanguliza wanaopigana na wewe, ili waonekane wako mbele yako, wengine wanasema, ‘huna elimu’, wengine wanasema, ‘miaka imepita na hujaolewa’, wengine wanasema, ‘wengine wenye umri wako wameshajenga nyumba’, hey hey hey Peninnah anakudharau lakini wewe badala ya kuwajibu, endelea kutazama kwake yeye Alpha na Omega wa imani yetu.


Tunasikia tu kwamba Penninah alikuwa na watoto lakini hayakutajwa, lakini Hannah alipopewa mtoto wake Samweli nchi yote ilimjua na mpaka sasa tunaongea juu ya Samweli. Nduguwe nisikilize, Mungu hana tabia yakutenda mambo kwa wakati unaotarajiwa na watu lakini anasubiria watu wakudharau kwanza wakucheke, wakupe jina la utani.


Mnaweza kucheka mnavyotaka lakini Mungu wangu akianza kutenda mambo yake kwangu mtaona mtoto wangu akitawaza wafalme. Kuchelewa kuzaa kwangu haimaanishi mimi ni mgumba, lakini kitu nilichobeba ni cha namna ya kipekee na kinakuja muda wa Mungu ukifika. Usijidharau na usijilinganishe na wengine kwa sababu wewe si wakawaida. Ni wa Kipekee!
Kwa kweli utazaa mtoto wa kipekee!. Uende kanisani!

SAIDIA RAFIKI YAKO KWA KUSAMBAZA HII HABARI!

Ilipitishwa na Apostle Pride Sibiya.

Be In Church!

HELP A FRIEND BY SHARING AS I HAVE DONE

Do you agree? Talk to me in the comments below!


Receive Jesus Christ today and go to church for spiritual fellowship.


Follow Apostle Pride Sibiya (Bishop: Glory Ministries) on Facebook, YouTube, Twitter, Periscope, WhatsApp, Google+, Instagram, Instaclips, and all social media.

Copyright: Brand Pride Sibiya (tempering with the article without permission of Brand is a criminal offense).

The views shared in this article may not necessarily be the same as those of the brand.
avatar
Bishop Pride Sibiya Online
This Is Bishop Pride Sibiya (www.pridesibiya.com) Official Website and Blog. Pride Sibiya Is An Apostle, Author, Blogger, Speaker, and The Founder and President Of Glory Ministries. Bishop Pride Sibiya
Chat with WhatsApp